#Football #Sports

KOCHA METTE ATOA TATHMINI KWA TUSKER FC

Kocha wa Tusker FC, Julien Mette, ametoa tathmini ya wazi kuhusu kikosi chake licha ya kuibuka na ushindi katika michezo miwili mfululizo iliyowasaidia kurudisha morali ya timu.

Ushindi huo ni pamoja na 2–0 dhidi ya Bidco United katika FKF Mozzart Bet Cup, matokeo yaliyoihakikishia Tusker nafasi ya hatua ya 16 bora na kuendeleza msururu wa mafanikio ya hivi karibuni katika mashindano mbalimbali.

Ingawa matokeo yameanza kuboreka, Mette amesisitiza kuwa hawezi kuridhika na bado kikosi chake kitalazimika kufanya zaidi ili kudumisha maendeleo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *