RUTO: NITAKOMBOA UKAMBANI KUTOKA UPINZANI
Ziara ya Rais William Ruto katika eneo la Ukambani iniangia siku ya 2 hii leo huku rais akitoa wito kwa eneo hilo kushirikiana naye kwenye uchaguzi mkuu ujao, akisema eneo hilo limekuwa kwenye upinzani kwa muda mrefu.
Alikuwa akizungumza kwenye kaunti ya Makueni alikoanzia ziara yake hapo jana, akitumia ziara hiyo kutetea ushuru unaotozwa wakenya na serikali yake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































