RUTO AMWAGIZA IG KUMALIZA UHUNI
Macho yote sasa yameelekezwa kwa idara ya polisi kuanzisha msako na kuwakamata washukiwa wa uhuni ambao wamekuwa wakivuruga mikutano ya kisiasa kote nchini, mwathiriwa wa hivi punde akiwa aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua Jumapili iliyopita.
Akitoa amri yake, Rais William Ruto amemwagiza Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja kuhakikisha washukiwa wote wanakamatwa ili kulihakikishia taifa utulivu.
Naye Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen, amesema magenge hayo hayatavumiliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































