DCP YAJIONDOA KWENYE UCHAGUZI MALAVA
Mwaniaji wa kiti cha ubunge kwenye uchaguzi mdogo unaokuja mwezi ujao eneo bunge la Malava Seth Panyako, amepigwa jeki baada ya chama cha DCP chake Rigathi Gachagua kumwondoa mwaniaji wake ili kumuunga mkono Panyako wa DAP-K.
Akitoa tangazo hilo, naibu kinara wa DCP Cleophas Malala, amesema muungano wa upinzani uliafikiana kumwasilisha mgombea mmoja ili kumenyana na yule wa chama tawala cha UDA David Ndakwa.
Haya yanajiri huku viongozi wa Kenya Kwaza wakimpigia debe Ndakwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































