#Football #Sports

JUNIOR STARS WAJIANDAA KWA S SUDAN

Timu ya taifa ya soka ya vijana wasiozidi umri wa miaka 17 Junior Stars wanajiandaa kwa mechi yao ya 3 hii leo dhidi ya South Sudan, baada ya ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya Rwanda kwenye mechi za kufuzu dimba la AFCON kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17.

Meneja mkuu wa kikosi hicho William Muluhya, amesema lengo ni kumaliza kileleni mwa kundi lao na kufuzu kwa kipute hicho.

Kwa sasa Junior Stars wana pointi 4 kufuatia ushindi mmoja na sare kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Somalia, na mechi yao ya mwisho itakuwa dhidi ya wenyeji Ethiopia.

Timu 3 kutoka baraza la CECAFA zitapata fursa ya kushiriiki AFCON U17 nchini Morocco.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

JUNIOR STARS WAJIANDAA KWA S SUDAN

EZE AIMARISHA MATUMAINI YA ARSENAL EPL

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *