#Business

AFUENI  KWA WAFANYABIASHARA BAADA YA UJENZI WA BARABARA KUZINDULIWA NAKURU

Wafanyibiashara katika eneo bunge la Kuresoi North kaunti ya Nakuru wana kila sababu ya kutabasamu baada ya Rais William Ruto kuzindua rasmi ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 12 ya Kinamba-Murinduku.

Barabara hiyo inatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa mazao, ikiwa ni pamoja na vitunguu, nyanya, pareto na mboga na wakati huo huo kuwaletea wakulima mapato kutokana na shughuli zao za kilimo.

Aidha, Rais Ruto ameahidi kwamba serikali yake iko mbioni kufanikisha mipango ya ujenzi wa barabara kuu ya Nairobi-Mau Summit ili kupiga jeki sekta ya uchumi na kumaliza msongamano wa magari.

Hata hivyo, uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kinamba-Murindiku umekuja wakati ambapo viongozi wa kaunti Nakuru wamekuwa wakitoa lalama kuhusu uwepo wa barabara mbovu ambazo zimefanya iwe vigumu kwa wakulima kusafirisha mazao yao hadi sokoni.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

AFUENI  KWA WAFANYABIASHARA BAADA YA UJENZI WA BARABARA KUZINDULIWA NAKURU

CARABAO YAINGIA RAUNDI YA 4

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *