#Rugby #Sports

HSBC SEVENS YAPATA UFADHILI ZAIDI

Shindano la HSBC Sevens, linalotarajiwa kufanyika wiki hii katika Uwanja wa Taifa wa Nyayo, limepata msaada mkubwa baada ya kampuni ya mawasiliano Safaricom, kupitia chapa yake ya M-PESA, kutoa KSh10 milioni kwa ajili ya hafla hiyo.

Victor Odada, Kiongozi wa Ushirikiano na Mipango  wa M-PESA, amesisitiza umuhimu wa kushiriki kwa wakenya wote katika mashindano haya, akiwataka mashabiki kuja kwa wingi kuunga mkono timu za taifa –Shujaa na Lionesses.

Ufadhili huo utajumuisha vivutio vya fedha taslimu  kusaidia kupunguza gharama za chakula na usafiri kwa mashabiki waliopo kwenye mechi, huku Odada akihimiza wananchi kushiriki pia kupitia kutazama michezo hiyo kote nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *