IEBC: HAKUNA WAPIGA KURA WAPYA
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imepuzilia mbali madai kwamba wapiga kura wapya wamesajiliwa katika maeneo kutakakofanyika chaguzi ndogo hapo kesho ili kufanikisha wizi wa kura, ikisema hakuna wapiga kura wapya walio na uwezo wa kushiriki zoezi hilo.
Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Marijan Hussein Marijan, amekariri kuwa sajili itayotumika ni ile ya mwaka 2022.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































