#Football #Sports

TUSKER WAWAROVYWA APS BOMET, GOR-UNITED KUSUBIRI

Kamati ya ligi na ushindani chini ya shirikisho la FKF inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu mechi iliyositishwa kati ya Gor Mahia na Nairobi United baada ya mashabiki kurusha vifaa uwanjani katika kipindi cha pili na kulazimu wasimamizi kuisitisha.

Kizaazaa hicho kilitokea mechi hiyo iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu ikiwa bao 1-1 katika dakika ya 58, wasimamizi wakisema mazingira katika uwanja wa Dandora hayakuwa salama kwao na wachezaji.

Katika mechi nyingine, Tusker FC walipanda kileleni mwa ligi kufuatia ushindi mgumu wa bao 1-0 dhidi ya APS Bomet ugani Kericho Green Stadium.

Bao la Dennis Oguta lilitosha kuwarovya maafande, na kuvunja msururu wa matokeo duni kwa Tusker FC.

Wakati uo huo, Bandari FC walitamatisha msururu wa mechi 5 bila ushindi baada ya kuvuna ushindi mwembamba dhidi ya Mathare United katika uwanja wa Mbaraki Sports Ground jijini Mombasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

TUSKER WAWAROVYWA APS BOMET, GOR-UNITED KUSUBIRI

ODM YATOA MASHARTI KWA KENYA KWANZA

TUSKER WAWAROVYWA APS BOMET, GOR-UNITED KUSUBIRI

MOROCCO WAANZA AFCON KWA USHINDI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *