#Local News

EACC, NG-CDF ZAJADILI KUZIBA UFISADI

Katika juhudi za kuziba mianya ya ufujaji wa fedha za umma katika hazina za kustawisha maeneo bunge, NG-CDF, tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC inafanya kikao na maafisa wa NG-CDF kutoka magharibi mwa nchi.

Mkutano huo unafanyika jijini Nakuru, mratibu wa EACC ukanda wa Magharibi Eric Ngumbi, akisema lengo ni kusaka suluhu kwa mianya hiyo ili kuzuia ufujaji wa fedha za umma.

Miongoni mwa mianya hiyo ni utoaji wa basari kwa wanafunzi hewa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *