#Local News

DUALE: WANAOGOMA SI WAHUDUMU WA AFYA

Vuta nikuvute baina ya wizara ya afya na wahudumu wa afya imechukua mkondo tofauti, Waziri wa Afya Aden Duale sasa akiwalaumu wahudumu hao na kudai kuwa wengi wanaogoma si wahudumu wa afya ila ni watu wasiofahamika wanaoingilia maandamano ili kuhujumu sekta ya afya.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Duale ametetea utendakazi wake, akisema ametatua changamoto za muda mrefu katika sekta hiyo zikiwemo za wahudumu wa afya ya wote UHC walioajiriwa wakati wa COVID-19.

Kauli yake imejiri baada ya maafisa wa kliniki kutishia kugoma kuanzia tarehe 23 mwezi huu kumshinikiza Duale kutia Saini makubaliano yao ya kurejea kazini.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

DUALE: WANAOGOMA SI WAHUDUMU WA AFYA

KNCHR YAPUZILIA MBALI CHAGUZI 

DUALE: WANAOGOMA SI WAHUDUMU WA AFYA

RIPOTI YAONYESHA JINSI MUMBE ALIVYOUAWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *