KESI YA CHUKI DHIDI YA SALASYA KUENDELEA, MAHAKAMA
Kesi ya kuhusu matamshi ya uchochezi inayomkabili mbunge wa Mumias East Peter Salasya itasikilizwa kikamilifu na mahakama na wala haitatatuliwa nje ya mahakama.
Katika kikao cha leo, hakimu Paul Mutai ametoa uamuzi huo baada ya mazungumzo ya upatanishi baina ya mbunge huyo na tume ya utangamano wa kitaifa NCIC kufeli, kesi hiyo sasa ikirataibiwa kusikilizwa tarehe 17 mwezi Januari mwaka ujao.
Kiongozi wa mashtaka hayo Virginia Kariuki, amesema NCIC haingeongoza upatanisho huo ikizingatiwa kuwa muda wake wa kuhudumu umetamatika na hivyo haina mamlaka kisheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































