#Local News

MGAO WA ELIMU KUONGEZEWA KSHS 65B, RUTO

Sekta ya elimu nchini inataratajiwa kuboreshwa katika kipindi cha mwaka mmoja ujao kutokana na mpango wa serikali kuongeza mgao wa sekta hiyo kwa shilingi bilioni 65 kwenye mwaka wa kifedha wa 2026-27.

Kulingana na Rais William Ruto, nyongeza hiyo ni sehemu ya mpango wa kuboresha sekta ya elimu, akisema serikali yake inaendelea kufanikisha utekelezaji wa mtaala wa CBE ili kuimarisha uwezo wa vijana kushindana katika soko la ajira.

Naye Waziri wa elimu Julius Ogamba, amewataka wakuu wa shule kuwasajili watahiniwa wote wa mitihani ya kitaifa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MGAO WA ELIMU KUONGEZEWA KSHS 65B, RUTO

NPS YATAKA MABILIONI ZA UCHAGUZI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *