BAYERN NA MAN UNITED WANG’ARA USIKU WA LIGI YA MABINGWAYA WANAWAKE
Klabu ya Bayern Munich ilipindua matokeo kwa kishindo baada ya
kutoka nyuma kwa mabao mawili na kuishinda Arsenal mabao 3–2
katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake usiku wa
Jumatano.
Arsenal walionekana kuwa na udhibiti kamili wa mchezo kupitia bao
la kichwa la mapema la Emily Fox na shuti kali la Mariona Caldentey
dakika ya 23, lakini Bayern walipambana kufa na kupona kipindi cha
pili.
Alara alianza kurejesha matumaini dakika ya 67, kabla ya mchezaji wa
akiba Pernille Harder kusawazisha kwa mkwaju maridadi, na Glodis
Viggosdottir kukamilisha kisasi dakika nne kabla ya mchezo
kumalizika kupitia krosi ya Klara Buehl.
Wakati huo huo, Manchester United waliandika historia kwa ushindi
wao wa kwanza wa Ulaya 2–1 dhidi ya Paris Saint-Germain kwenye
Uwanja wa Old Trafford, katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa kuchezwa huko badala ya Leigh Sports Village.
Melvine Malard alifungua ukurasa kwa bao zuri lililomshinda mlinda
lango wa zamani wa United Mary Earps, kabla ya Olga Carmona
kusawazisha kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Kisha, baada ya maandalizi mazuri yaliyoongozwa na Jess Park, Anna
Sandberg alipiga krosi safi iliyomkuta Fridolina Rolfo, ambaye alifunga
bao la ushindi dakika ya 58 — ushindi huo umewafanya United
kushinda mechi tatu kati ya tatu katika kampeni yao ya kwanza ya Ligi
ya Mabingwa ya Wanawake.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































