WAZAZI: SERIKALI ILITUDANGANYA
Baadhi ya wasimamizi wa shule mbali mbali za upili wamepuzilia mbali agizo la Rais William Ruto la kuwataka wanafunzi wa grade 10 waripoti shuleni bila kujali iwapo wana sare na karo au la, wazazi sasa wakihisi kuhadaiwa na serikali.
Wengi wa wanafunzi hasa katika mitaa ya mabanda wamesalia nyumbani kutokana na ukosefu wa karo na mahitaji mengine ya shule, wazazi wakisema walirejeshwa nyumbani na usimamizi wa shule.
Kulingana na Waziri wa elimu Julius Ogamba, asilimia 98 ya wanafunzi wa grade 10 wameripoti shuleni.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































