MHOLANZI ALIYEMSHAMBULIA POLISI AACHILIWA
Raia wa Uholanzi Elwin Ter Horst aliyekamatwa wiki 2 zilizopita kwa makosa ya kumshambulia afisa wa polisi katika eneo la Diani kaunti ya Kwale, ameachiwa bila masharti yoyote baada ya mahakama kubaini kuwa ana matatizo ya msongo wa mawazo yaani bipola na hivyo hawezi kujibu mashtaka.
Hakimu mwandamizi Joy Mutimba, ametoa uamuzi huo baada ya kupokezwa ripoti ya matibabu, inayoonyesha kuwa mshtakiwa ana matatizo hayo na mengine ya kiafya yanayomzuia kujibu mashtaka.
Kulingana na stakabadhi za mahakama, Ter Horst alikuwa akikabiliwa na mashtaka 4 ikiwemo kusababisha usumbufu, uharibifu wa mali kimaksudi na ulanguzi wa dawa za kulevya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































