WAATHIRIWA WA MAPOROMOKO CHESONGCH KUZIKWA LEO
Watu 31 walioangamia kwenye maporomoko ya ardhi katika eneo la Chesongoch kaunti ya Elgeyo Marakwet wameratibiwa kuzikwa hii leo katika kaburi la pamoja, huku wengine 4 wakizikwa na familia zao kwenye mashamba yao.
Watu 32 zaidi wanaendelea kuuguza majeraha kutokana na maporomoko hayo huku wengine 9 wakikosa kujulikana waliko, na zaidi ya familia 600 zikiachwa bila makao.
Waathiriwa wameitaka serikali kuwatafutia makazi mbadala.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































