#Local News

KANJA AKATA RUFAA DHIDI YA UAMUZI WA KUZUIA USAJILI

Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja amewasilisha rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kuu kusitisha kwa muda zoezi la usajili wa makurutu wa kujiunga na idara ya polisi, akitaka amri hiyo ifutiliwe mbali.

Kwenye ombi lake, Kanja ametaja usitishwaji huo kuwa hatari, ikizingatiwa kuwa idara ya polisi inalenga kuimarisha usalama, akiitaka mahakama kuzingatia sheria inayoitaka idara hiyo kujiandaa mapema kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Kesi ya kupinga zoezi hilo iliwasilishwa na mwanaharakati Eliud Matindi, anayesema kuwa ni jukumu la NPSC kuwaajiri polisi na wala si Inspekta mkuu wa polisi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *