TAMASHA LA RAGA YA WANAWAKE 10-A-SIDE KUREJEA RFUEA
Tamasha la Raga ya Wanawake 10 kila upande chini ya shirikisho la
raga nchini litarejea rasmi Jumamosi, Januari 31, mwaka huu katika
Uwanja wa RFUEA jijini Nairobi, likitarajiwa kuleta siku nzima ya raga
ya kasi na ushindani mkali.
Mashindano hayo yatahusisha timu 10 kutoka maeneo mbalimbali
nchini na ni sehemu muhimu ya maandalizi kuelekea msimu wa Ligi ya
Kenya Cup Wanawake 2026 itakayoanza Februari 7.
Tamasha hilo limekusudiwa kutoa jukwaa la kukuza vipaji pamoja na
kupima ushindani, huku timu chipukizi zikipewa nafasi ya kuonyesha
uwezo wao na zile zilizozoeleka zikitumia mashindano hayo kunoa
mifumo yao kabla ya kuanza kwa ligi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































