UCL: INTER MILAN KUTAFUTA USHINDI DHIDI YA BODO GLIMT
Ligi kuu ya mabingwa barani ulaya hatua ya mwondoano itarejelewa hii leo kwa mkondo wa pili huku mechi kadhaa zikiratibiwa kuchezwa, Inter Milan watakua nyumbani San Siro wakitafuta kubatilisha matokeo ya wiki iliyopita walipochapwa mabao 3-1 na Bodo Glimt. Inter lazima washinde mchezo wa leo ili kufuzu hatua nyingine. Mechi nyingine zitakazochezwa ni pamoja na Newcastle dhidi ya Qarabaq, Leverkusen wagaragazane na Olympiacos huku Atletico Madrid wakicheza na Club Brugge.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































