BRANDON OBIERO AWEKA LENGO LA KIPA BORA ZAIDI NCHINI
Kipa wa Tusker, Brandon Obiero, anasema anatamani kuwa miongoni mwa makipa bora nchini baada ya kupata nafasi ya kuanza mechi mbili mfululizo kwenye Ligi kuu ya Kenya.
Obiero ameanza dhidi ya Mara Sugar na Ulinzi Stars, akihifadhi clean sheet katika mechi zote mbili ambazo Tusker ilishinda 1–0.
Mchezaji huyo aliyejiunga na Tusker mwanzoni mwa msimu akitokea Talanta FC, anasema ametimiza malengo makubwa na ataendelea kujisukuma zaidi ili kufikia viwango vya juu katika kampeni iliyosalia.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































