MVUA KUPUNGUA ILA HATARI INGALIPO- UBASHIRI
Kiwango cha mvua inayonyesha nchini kimebashiriwa kupungua wiki hii ila hatari ya mafuriko itaendelea, wakenya wakitakiwa kuchukua tahadhari na kuhamia nyanda za juu.
Kupitia taarifa, idara ya hali hewa imesema licha ya mvua kupungua, ardhi nyingi haziwezi kustahimili maji zaidi kutokana na mvua kubwa katik wiki za hivi karibuni, na hivyo manyunyu pekee yanaweza kusababisha mafuriko na mapromoko ya ardhi.
Kulingana na idara hiyo, maeneo yatakayoendelea kupokea mvua ni ukanda wa Ziwa Victoria, Rift Valley na Nairobi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































