NTSA YATANGAZA MSAKO BARABARANI
Wasafiri wamehakikishiwa usalama wao barabarani hasa msimu huu wa Krisimasi, mamlaka ya usalama barabarani NTSA ikitangaza msako mkali dhidi ya madereva wanaokiuka sheria za trafiki.
Kwenye msako huo, NTSA itategemea mahakama tamba zitakazohakikisha kuwa madereva wanaokamatwa wanashtakiwa na kuhukumiwa papo hapo, mbali na utekelezaji wa vifaa vya kudhibiti mwendo.
Aidha, wakenya wameruhusiwa kurekodi video za maafisa wa trafiki wanaochukua hongo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































