KNEC YAONYA KUHUSU USAJILI WA KCSE 2026
Baraza la Kitaifa la Mitihani nchini, KNEC, limeonya kuwa hakutakuwa na usajili wa kuchelewa kwa watahiniwa wanaotarajia kufanya mtihani wa KCSE mwaka 2026.
Kupitia taarifa, KNEC imesema usajili wa mtihani huo ulianza Februari 16 na unatarajiwa kufungwa rasmi Machi 31 bila kuongezwa muda zaidi.
Baraza hilo pia limeeleza kuwa mtihani wa KCSE wa mwaka 2026 utakuwa wa pili kutoka mwisho kufanywa chini ya mfumo wa elimu wa 8-4-4 kabla ya nchi kuhamia kikamilifu katika mfumo wa mtaala wa umahiri, CBC
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































