VIONGOZI, MATAIFA YAPONGEZA UCHAGUZI WA PROF. OKOWA
Uchaguzi wa Prof. Phoebe Okowa kuhudumu kama jaji wa mahakama ya kimataifa kuhusu haki ICJ umeendelea kupongezwa na viongozi na nchi mbali mbali, akiwa ni mwanamke wa kwanza kutoka Kenya kuchaguliwa kwenye wadhifa huo.
Wa hivi punde ni mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, katibu katika wizara ya masuala ya kigeni Korir Sing’oei na mataifa yakiwemo Colombia.
Prof Okowa anachukua mahali pa hakimu Abdulqawi Yusuf wa Somalia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































