#Football #Sports

UFARANSA WATINGA KOMBE LA DUNIA, NORWAY NA URENO ZIKISUBIRI

Timu ya taifa ya soka ya Ufaransa imetinga kipute cha kombe la dunia kitakachoandaliwa mwaka ujao, kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ukraine jana usiku, mechi iliyosakatwa wakati Ufaransa ikiadhimisha miaka 10 tangu shambulizi la kigaidi la mwaka 2015.

Mechi hiyo iliyojawa na hisia za ukumbusho iliandaliwa katika uwanja wa Parc des Princes, mabao yakipachikwa wavuni na Hugo Etikite katika kipindi cha kwanza na Kyllian Mbappe na Michael Olise katika kipindi cha pili, yakiwapa vijana hao wa Didier Deschamps uongozi wa pointi 6 katika Group D ambayo inajumuisha Iceland, na Azerbaijan.

Ufaransa sasa wanaangazia droo ya kipute cha kombe la dunia itakayoandaliwa jijini Washington DC tarehe 5 mwezi ujao, kufahamu wapinzani wao katika awamu ya makundi huku Ukraine na Iceland wakimenyana Jumapili kusaka tiketi ya kushiriki mwondoano yaani playoff.

Wakati uo huo, Norway yake Erling Haaland ilivuna ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Estonia, Haaland akitinga magoli mawili na ku.

Hata hivyo, ushindi wa dakika za mwisho wa Italia dhidi ya Moldova unamaanisha Norway watasubiri hadi mechi ya mwisho dhidi ya Italia kabla ya kufuzu, ingawa kwa Italia kumaliza wa kwanza, watahitaji kupata ushindi wa zaidi ya mabao 17, tukio ambalo halijashuhudia katika historia ya hivi karibuni ya soka.

Katika matokeo mengine, Ureno yake Cristiano Ronaldo pia iliwekwa kwenye waiting bench baada ya kupokezwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Ireland.

Ronaldo iliondolewa mchezoni kwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu, Ureno sasa ikisalia kwa pointi 10, 3 mbele ya Ireland na 2 mbele ya Hungary, waliopata ushindi wa goli 1-0 dhini ya Armenia.

Mechi ya mwisho ya Ureno itakuwa nyumbani dhidi ya Armenia Jumapili hii, Hungary wakiwakaribisha Ireland katika kile kitakachoonekana kuwa kuwinda nafasi ya pili.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UFARANSA WATINGA KOMBE LA DUNIA, NORWAY NA URENO ZIKISUBIRI

EAGLES WA NIGERIA WAPAA HADI FAINALI

UFARANSA WATINGA KOMBE LA DUNIA, NORWAY NA URENO ZIKISUBIRI

MHOLANZI ALIYEMSHAMBULIA POLISI AACHILIWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *