MAHAKAMA YASITISHA MAKUBALIANO TATA YA KENYA-MAREKANI
Mahakama kuu imetia breki utekelezaji wa mkataba wenye utata wa ushirikiano katika sekta ya afya uliotiwa Saini kati ya Kenya na Marekani, hadi kesi iliyowasilishwa na seneta wa Busia Okiya Omtata itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Kwenye uamuzi wake, jaji Lawrence Mugambi amewazuia washtakiwa kwenye kesi hiyo kutekeleza, kuanzisha matumizi ya sehemu yoyote ya mkataba huo unaohusisha uhamisho, na kutuma kwa deta za kibinafsi za afya.
Omtatah aliwasilisha kesi hiyo mahakamani hapo jana, akihoji kuwa wakenya hawakuhusishwa inavyohitajika kisheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































