These anal toys arent just about pleasurethey additionally

Buy Adult Intercourse Toys On-line With Confidence: We Guarantee Your Satisfaction! In addition osexlove, the tiny sex toy is also used to stimulate different erogenous zones just like the nipples, internal thighs, and your partner’s balls. Let’s move on to the design next, the place our testers loved the slender head (highlighted within the picture […]

ODM:TUNGALA IMARA NA MAARUFU

Uongozi wa chama cha ODM umesisitiza kuwa chama hicho kingali imara kutokana na ushindi wake wa viti vya ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa hapo jana, ukisema chama hicho kitaunda serikali baada ya uchaguzi mkuu ujao. Wakiongozwa na naibu kinara wa chama hicho Abdulswamad Nassir na mwenyekiti wa kitaifa Gladys Wanga, ODM imehusisha ushindi huo pia […]

KARISH ATISHIA KUPINGA USHINDI WA WA  MUTHENDE

Aliyekuwa mgombeaji wa ubunge katika eneo la Mbeere North kwa tiketi ya chama cha DP Newton Karish, ametishia kupinga ushindi wa mbunge mteule eneo hilo Leo wa Muthende mahakamani, kutokana na tofuati za majina katika vifaa vya KIEMS na karatasi za kupigia kura. Kupitia kwa wakili wake Ndegwa Njiru, Karish ameibua madai kwamba tume ya […]

SERIKALI KUIMARISHA USHIRIKIANO NA CHINA KUBORESHA MIUNDOMBINU

Rais William Ruto amesema serikali yake itaendelea kuimarisha ushirikiano na China katika hali ya ushirikiano na maendeleo ya pamoja.Ruto, ambaye alikuwa mwenyeji wa ujumbe kutoka Benki ya Exim-Import ya China (China Exim Bank) ukiongozwa na Mwenyekiti Chen Huaiyu jijini Nairobi, amesema kuongezeka kwa uwepo wa kampuni za Kichina nchini Kenya kunaonyesha imani yao katika utulivu wa nchi na […]

RUTO ATASHINDA MSIPOREKEBISHA, VIJANA WAONYWA

Rais William Ruto atashinda uchaguzi mkuu ujao kwa kishindo iwapo vijana wataendelea kukosa kujitokeza kupiga kura jinsi ilivyoshuhudiwa kwenye chaguzi ndogo hapo jana. Haya ni kwa mujibu wa washikadau katika sekta ya elimu wakiongozwa na Synthia Asienwa, wakihimiza haja ya uhamasisho kufanywa kuhusiana na umuhimu wa kushiriki uchaguzi. Wamekuwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha […]

KOMBE AREJESHWA MAMLAKANI MAGARINI 

Mgombeaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi kwa tiketi ya ODM Harrison Kombe, ameibuka mshindi kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika eneo hilo hapo jana. Kulingana na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, Kombe amepata jumla ya kura 17,909, dhidi ya mshindani wake Stanley Kenga wa DCP aliyepata kura 8,907. […]

SLOT ASISITIZA ATAINUSURU LIVERPOOL

Meneja wa klabu ya Liverpool Arne Slot ameapa kuendelea kupambana,akisema mazungumzo kati yake na wamiliki wa Liverpool haijabadilika licha ya matokeo duni yanayoendelea kuandikishwa na klabu hiyo. Mabingwa hao wa EPL walipepetwa magoli 4-1 na PSV Eindhoven kwenye dimba la klabu bingwa bara Ulaya Jumatano, kikiwa kichapo chao cha 9 katika mechi 12 zilizopita. Hatua […]

SERIKALI KUWAZADI MAGWJI WA DEAFLYMPICS

Serikali inatarajiwa kutuza kikosi kilichowakilisha Kenya katika mashindano na Deaflympics jijini Tokyo, Japan na shilingi milioni 36 baada ya kikosi hicho kutia fora katika mashindano hayo na wanamichezo wasio na uwezo wa kusikia. Akizungumza baada ya kuwakaribisha nchini wanamichezo hao katika uwanja wa JKIA, katibu mkuu katika wizara ya michezo Elijah Mwangi amesema serikali itawatuza […]

LINDAH KIHARA NGUZO YA KAYOLE STARLETS, MKUFUNZI

Kocha mkuu wa klabu ya Kayole Starlets inayoshiriki ligi kuu ya wanawake nchini Mary Adhiambo, amemtaja mshambulizi wa klabu hiyo Lindah Kihara kama nguzo kwa timu hiyo, kutokana na mchezo wake wa kufana msimu huu. Fowadi huyo amekuwa katika ubora wake, akifunga mabao 3 na kuchangia bao 1 katika mechi 6 za ligi, mchango ambao […]

NDAKWA AAHIDI USHIRIKIANO

Mbunge mteule wa Malava kaunti ya Kakamega David Athman Ndakwa, ameahidi kuwashirikisha wakazi wote eneo hilo katika uendeshaji wa majukumu yake, bila kuzingatia tofauti za kisiasa. Akizungumza baada ya kupokezwa cheti cha ushindi kwenye uchaguzi mdogo, Ndakwa ameipongeza IEBC akisema imeendesha uchaguzi huo kwa mujibu wa mwongozo wa sheria. Imetayarishwa na Antony Nyongesa