STARS WALENGA KUJINUSURU NA TANZANIA
Timu ya taifa kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 Junior Stars watamenyana na Tanzania katika awamu ya semifainali ya mashindano ya kufuzu dimba la klabu bingwa barani Afrika AFCON kupitia ukanda wa CECAFA, licha ya kichapo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ethiopia.
Licha ya kichapo hicho, Stars walimaliza wa pili katika Group A, kutokanna sare ya bao 1 dhidi ya Somalia, na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Rwanda, na watakabiliana na mshindi wa Group B ambaye ni jirani Tanzania.
Matineja hao wangali na nafasi ya kufuzu AFCON U17 mwaka ujao nchini Morocco, iwapo watailaza Tanzania.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































