28 WAJERUHIWA KWENYE AJALI NAKURU
Watu 28 wanauguza majeraha, 12 kati yao wakiwa katika hali mahututi baada ya kuhusika kwenye ajali katika eneo la Salgaa kwenye barabara ya Nairobi- Nakuru mapema leo.
Kulingana na shirika la Red Cross, basi hilo linalomilikiwa na kampuni ya Easy Coach lilikuwa likitoka Nairobi kuelekea Kisumu lilipogonga lori la kusafirisha mizigo na kusababisha ajali hiyo.
Red Cross imesema 12 hao walipelekwa haraka hospitalini ila 16 wakahudumiwa katika eneo la mkasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































