#Business

KENYA YAIPIKU NIGERIA KUONGOZA UKUAJI WA SEKTA YA KIBINAFSI AFRIKA

Kenya imerekodi mafanikio makubwa zaidi ya sekta ya kibinafsi kati ya mataifa makubwa ya kiuchumi barani Afrika mwezi Novemba, na kuongoza safu ya PMI ya S&P Global kwa alama 55.0.

Kufuatia ripoti ya Finance in Africa, taarifa hiyo inaashiria ukuaji wa haraka zaidi katika miaka mitano, ukichochewa na kuongezeka kwa mauzo, maagizo mapya ya wateja, na kupunguza shinikizo la bei. Uganda ilifuatia kwa PMI ya alama 53.8, huku Nigeria ikishika nafasi ya tatu kwa 53.6, ikiendeleza msururu wake wa upanuzi hadi miezi 12.

Zambia, Misri, Msumbiji, na Ghana pia zilichapisha usomaji zaidi ya alama 50, kuashiria maboresho ya kawaida, wakati Afrika Kusini ilisalia kuwa uchumi pekee uliodorora. PMI juu ya 50 inaonyesha ukuaji.Benki ya Dunia inasema ufufuaji wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara unaimarika, huku ukuaji wa Pato la Taifa ukitarajiwa kupanda kutoka 3.5% mwaka 2024 hadi 3.8% mwaka 2025, ukisaidiwa na kudhibiti mfumuko wa bei na kuboresha hali ya biashara katika kanda nzima.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

KENYA YAIPIKU NIGERIA KUONGOZA UKUAJI WA SEKTA YA KIBINAFSI AFRIKA

MAKATO YA SHIF NA USHURU WA NYUMBA

KENYA YAIPIKU NIGERIA KUONGOZA UKUAJI WA SEKTA YA KIBINAFSI AFRIKA

KALONZO KUSITISHA UUZAJI WA HISA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *