BABAKE OJWANG’ ATAKA LAGAT AKAMATWE
Familia ya bloga na mwalimu Albert Ojwang’ aliyeuawa katika kituo cha Central Police jijini Nairobi sasa inamtaka naibu inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat akamatwe na kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya mwanao.
Katika hatikiapo mahakamani, babake Ojwang’, Meshack Ojwang’ anamtuhumu Lagat kwa kupanga utekaji nyara, mateso na mauaji ya mwalimu huyo mapema mwaka huu, akisema serikali ilijaribu kuwaficha wahusika akiwemo Lagat.
Ojwang’ analalamika kuwa licha ya ripoti ya upasuaji kuweka wazi kwamba mwanawe aliuawa na wala hakujiua, hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi ya afisa huyo mkuu wa polisi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































