SERIKALI YACHUNGUZA UDUKUZI DHIDI YAKE
Serikali inaendeleza uchunguzi katika tukio la udukuzi dhidi ya tovuti za wizara za maji, usalama, afya, leba na elimu na kuathiri kwa muda utoaji huduma kwa wananchi hapo jana.
Katibu mkuu katika wizara ya usalama Raymond Omollo, amehusisha udukuzi huo na kundi la PCP@Kenya, akiutaja udukuzi huo kuwa uvunjaji wa sheria.
Udukuzi wa hivi punde na mashambulizi mengine ya mtandaoni dhidi ya tovuti za serikali yanaathiri moja kwa moja uchumi wa kidijitali.
Imetayarishwa na Anytony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































