MVUA YA MAANGAMIZI
Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko kote nchini imethibitishwa kufikia watu 42, huku familia zikiachwa na hasara kutokana na uharibifu wa mali yakiwemo mashamba, nyumba na magari.
Takwimu za serikali zinaashiria kuwa zaidi ya familia 10,000 zimeathirika na mafuriko hayo, zaidi ya watu 4,000 wakilazimika kutafuta makazi katika maeneo salama.
Hata hivyo, Waziri wa utumishi wa umma na mipango maalum Geoffrey Ruku, amesema serikali inaendelea kutoa msaada.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































