NIGERIA WATINGA ROBO FAINALI AFCON
Super Eagles wa Nigeria walipaa juu kwa juu na kuingi robo fainali ya dimba la taifa bingwa barani Afrika AFCON 2025 baada ya kuwapepeta the Mambas wa Msumbiji kichapo cha mabao 4-0 nchin Morocco jana usiku.
Mshambulizi wa Galatasaray Viktor Osimhen alifunga mara 2, Ademola Lookman na Akor Adams wakifunga moja kila mmoja na kuwapa Super Eagles tiketi ya kutinga robo fainali, wakidumisha matumaini ya kurejea kwenye fainali jinsi ilivyokuwa mwaka wa 2024 ambako walibanduliwa na Ivory Coast.
Msumbiji ambao walikuwa kwenye awamu ya mwondoano kwa mara ya kwanza, walipata taabu kuwadhibiti Nigeria wanaojivunia makali ya safu ya ushambulizi na kasi ya viungo.
Nigeria watachuana na mshindi wa pambano la leo kati ya bingwa wa mwaka 2019 Algeria na DR Congo, na ikiwa watachuana na Kongo basi yatakuwa ni marudiano ya Novemba mwaka jana, ambapo Leopards walizima matumaini ya Nigeria kupata tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwaka huu.
Kwa upande mwingine, Misri yake Mo Salah itabaini mpinzani wake war obo fainali katika pambano jingine kati ya bingwa mtetezi Ivory Coast na Burkina Faso, baada ya kuwnayuga Benin 3-1 jana usiku.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































