#Local News

BABU OWINO MAHAKAMANI KUPINGA SHERIA

Mbunge wa Embakasi East Babu Owino na mkenya mwingine kwa jina Mwaura Kabata, wamewasilisha kesi mahakamani kupinga sheria iliyopitishwa maajuzi kuhusiana na mgongana wa maslahi ama conflict of interest inayowaruhusu mawaziri kujihusisha na siasa.

Kwenye kesi hiyo, walalamishi wanataka amri za muda kutolewa kufutilia mbali utekelezaji wa sehemu ya 25 ya sheria hiyo, wanayoitaja kuwa kinyume na katiba, ya ubaguzi na tishio kwa kanuni inayowazuia watumishi wa umma kuegemea mirengo ya kisiasa.

Wameitaka mahakama kumzuia mwanasheria mkuu, mawaziri na viongozi wengine wakuu serikalini kujihusisha na siasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

BABU OWINO MAHAKAMANI KUPINGA SHERIA

ODM?: HUENDA TUKAJIONDAO SERIKALINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *