#Football #Sports

NAIROBI UNITED KUMENYANA NA AZAM, MIAMBA

Klabu ya Nairobi United itamenyana na miamba wa Morocco Wydad Casablanca, AS Maniema ya DR Congo na Azam ya Tanzania kwenye kundi B la awamu ya makundi ya kipute cha klabu bingwa ya mashirikisho barani Africa, CAF Confederations Cup msimu huu wa 2025-26.

Droo ya makundi ambapo timu itacheza nyumbani na ugenini dhidi ya kila timu kwenye kundi, ilifanyika hapo jana nchini South Africa, sawa na ile ya klabu bingwa barani Afrika, CAF Champions League.

Awamu ya makundi inajumuisha timu 16 zilizofuzu kutoka kwenye awamu 2 za kufuzu, na zimegawanywa katika makundi 4.

Kundi A linajumuisha USM Alger (Algeria), Djoliba AC de Bamako (Mali), Olympique Club de Safi (Morocco), FC San Pedro (Cote d’Ivoire)

Aidha, Kundi C linawakutanisha CR Belouizdad (Algeria), Stellenbosch FC (South Africa), AS Otoho (Congo), Singida Black Stars (Tanzania)

Nalo kundi D litashuhudia kivumbi kati ya miamba wa Misri, Zamalek, Al Masry (Egypt), Kaizer Chiefs (South Africa), ZESCO United (Zambia)

Awamu ya makundi itaanza wikendi ya tarehe 21–23 mwezi huu, raundi zikiratibiwa kuskatwa kabla ya kipute cha mataifa bingwa barani Afrika AFCON kitakachoandaliwa nchini Morocco, kabla ya kurejelewa wikendi ya Januari 23–25, 2026.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

NAIROBI UNITED KUMENYANA NA AZAM, MIAMBA

WADAU WAONYWA DHIDI YA WIZI WA MTIHANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *