GUNNERS WAFUMWA NA THE BEES, WAYUMBA EPL
Washika bunduki wa Arsenal maarufu kama Gunners walishindwa kuhimili mishale ya nyuki wa Brentford jana usiku, na kupoteza nafasi ya kipekee ya kurejesha uongozi wa alama 6, ligi kuu ya soka nchini Uingereza, EPL ikishika kasi.
Bao la Keane Lewis-Potter katika dakika ya 71 ya mchezo lilididimiza matumaini ya Arsenal kubeba taji la EPL msimu huu, baada ya kufuta uongozi wao waliokuwa wamechukua kupitia kwa Noni Madueke kunako dakika ya 61.
Kwa sasa Arsenla, ambao wikendi iliyopita walikuwa waliongoza ligi kwa pointi 9 kwa muda, wako kileleni wakiiacha Manchester City na pointi 4 pekee, maswali yakiibuka kuhusu iwapo mtindo wa Gunners kuachilia uongozi saa za lala salama utaendelea, ama watawakatia kiu cha miaka 22 wafuasi wao ambao wameishi kutamani kutwaa ubingwa huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































