META, TIKTOK KUTII SHERIA ZA MIAKA 16 AUSTRALIA
Kampuni teknolojia za utoaji huduma za mitandao ya kijamii Meta na TikTok imetangaza kutii agizo la kuwazuia watoto walio chini ya umri wa miaka 16 nchini Australia kutumia mitandao hiyo, ingawa zikaonya kuwa huenda utekelezaji wa sheria hizo ukawa na changamoto.
Sheria hizo zitaanza kutekelezwa tarehe 10 mwezi Disemba, ambako watumiaji walio chini ya miaka 16 kiumri wataondolewa kwemye mitandao ya Facebook, TikTok na Instagram.
Inasubiriwa kwa hamu kuona iwapo Australia itafanikiwa kutekeleza marufuku hiyo, huku kampuni za tekonolojia zikipambana na athari za mitandao ya kijamii.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































