#Local News

HAJA YA MAFUNZO YA HUDUMA ZA KWANZA YAIBUKA

Wakenya wamehimizwa kupata mafunzo ya kutoa huduma za kwanza ili kupunguza maafa wakati wa mkasa au ajali katika maeneo ya mashinani kama ile ya ndege iliyotokea katika eneo la Mosop kaunti ya Nandi wikendi iliyopita.

Jacobeth Jeptoo, mwanafunzi wa uuguzi aliyejitolea kutoa huduma za kwanza kwa waathiriwa wa ajali hiyo iliyowaua watu 6, amesema mafunzo hayo yatasaidia kuokoa maisha.

Mwanafunzi huyo amegonga vichwa vya habari kutokana na juhudi zake kujaribu kuokoa maisha ya waathiriwa wa ajali hiyo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *