KPA MACHO SASA WBLA
Klabu ya mpira wa vikapu ya Kenya Ports Authority KPA imeimarisha maandalizi yake inapojiandaa kushiriki Ligi ya wanawake ya mchezo hio barani Afrika WBLA baadaye mwishoni mwa wiki hii nchini Misri.
KPA wanalenga kutumia uzoefu wao kujitangaza katika kiwango cha bara kwenye mashindano hayo.
Kwa mujibu wa naibu mkufunzi Samuel Ocholla, kikosi hicho kinalenga kutumia mbinu mpya na kurekebisha mapungufu yao ya awali kabla ya mtanange huo, akiongeza kuwa tayari wameanza mazoezi.
Amesema wanachoangazia pakubwa ni ukakamavu wao katika kipindi cha mwisho, akirejelea mashindano ya Zone Five yaliyokamilika majuzi ambapo kikosi chake kilipoteza wakati wa kipindi hicho na kumaliza wa 3 kufuzu WBLA.
Kipute hicho cha bara kitaanza Ijumaa hii na kukamilika tarehe 14.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































