WANAHARAKATI WAKEJELI ‘MAIGIZO’ TANZANIA
Watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi wa urais hii leo, huku mashirika ya kutetea haki za kidemokrasia yakimkosoa rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa madai ya ukiukaji wa haki hizo kutokana na hatua yake ya kuwafungia nje wawaniaji wa upinzani.
Wakiongozwa na kiongozi wa chama cha PLP Martha Karua, wameutaja uchaguzi huo kuwa maigizo na wala si uchaguzi.
Hata hivyo, tume ya uchaguzi nchini humo imesema iko tayari kuendesha uchaguzi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































