#Athletics #Sports

EDMUND SEREM KUANGAZIA HESHIMA YA KIMATAIFA

Mshindi wa medali ya shaba ya dunia katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji, Edmund
Serem, anaamini umaarufu wake mpya katika majukwaa ya kimataifa utampa msukumo muhimu
kuelekea msimu wa 2026 ambao anatarajia kuutawala.
Serem alitunukiwa tuzo ya World Athletics Rising Star of the Year wikendi iliyopita, kutambua
msimu wake bora wa 2025 uliodhihirisha ustahimilivu, maendeleo na ahadi yake kubwa kwenye
mbio za kuruka viunzi na maji . Tuzo hiyo imemuongezea kujiamini kwamba msimu ujao unaweza
kuwa bora zaidi.
Hata hivyo, Serem anasema anafahamu kwamba ni kazi na mazoezi ya kujituma yatakayohakikisha
anaendeleza mwelekeo wake mzuri kwenye mbio hizo na kubaki miongoni mwa wanariadha
wanaochipukia kwa kasi duniani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

EDMUND SEREM KUANGAZIA HESHIMA YA KIMATAIFA

SICHENJE: TUJIPANGE AFCON MAPEMA

EDMUND SEREM KUANGAZIA HESHIMA YA KIMATAIFA

PALMER KUTOCHEZA DHIDI YA ATALANTA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *