CA YAPUUZA MADAI YA KULAZIMISHA UKUSANYAJI WA DATA
Mamlaka ya mawasiliano nchini imepuuzilia mbali madai ya mamlaka hiyo kuwalazimisha wahudumu wa mtandao wa simu kukusanya data ya kibayometriki chini ya kanuni mpya za usajili za kadi za simu zilizorekebishwa nchini.
Katika taarifa iliyotolewa hii leo mdhibiti ametaja wasiwasi huo kuwa usio na msingi.
Mamalaka hiyo imefafanua kuwa sheria zilizosasishwa na kuchapishwa mnamo mei 2025 zinalenga kuwalinda wakenya dhidi ya ulaghai unaohusiana na kadi za simu, wizi wa vitambulisho, na aina nyinginezo za uhalifu wa kidijitali.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































