CHANGAMOTO ZA KPSEA, KJSEA
Mitihani ya kitaifa ya gredi ya 6 KPSEA na gredi ya 9 KJSEA inaingia siku ya pili hii leo huku changamoto kadhaa zikiripotiwa katika siku ya kwanza ya mitihani hiyo hapo jana.
Miongoni mwa changamoto hizo ni baadhi ya shule kukosa kuwasajili watahiniwa, huku wanafunzi katika shule ya Endikir kaunti ya Kajiado wakianza mtihani wao alasiri baada ya karatasi za mtihani kukosekana kwenye kasha la kuhifadhi mitihani.
Jumla ya watahiniwa milioni 3.4 wanafanya mtihani huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































