FAITH KIPYEGON KUONGOZA MBIO ZA 3000M MONACO
Mshindi mara tatu wa Olimpiki, Faith Kipyegon, amethibitishwa kuongoza mbio za wanawake wa mita 3000 katika hafla ya Herculis EBS Monaco itakayofanyika Julai 10, mwaka huu.
Kiungo huyo mahiri wa mbio za kati atarejea Stade Louis-II, miaka mitatu baada ya kuvunja rekodi ya dunia ya maili moja huko mwaka 2023, alipoanza kuibua hisia kwa mashabiki wa mbio za kimataifa.
Rekodi hiyo ilikuwa moja kati ya tatu za dunia alizovunja katika msimu wa 2023 wa Diamond League, ambao Faith aliutaja kama msimu wake bora zaidi hadi sasa, na pia moja kati ya rekodi tano za dunia alizoweka kwenye mashindano ya Diamond League katika miaka mitatu iliyopita.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































