#Local News

KIZZA BESIGYE AHAMISHWA HOSPITALINI KUFUATIA HALI MBAYA YA AFYA

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Dkt. Kizza Besigye, aliondolewa gerezani na kukimbizwa hospitalini baada ya afya yake kudorora na kufikia hali hatari usiku wa kuamkia Jumanne.

Besigye, kiongozi wa PFF, amekuwa gerezani kwa muda na alipokuwa akikimbizwa hospitalini, msafara wake uliandamana na maafisa wengi wa usalama.

Chama chake kimeshutumu serikali kwa kumnyima Besigye huduma bora za kimatibabu, na kuendelea kuzuiliwa kwake kumeelezwa kuwa ni kumenyima haki zake za kimsingi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

KIZZA BESIGYE AHAMISHWA HOSPITALINI KUFUATIA HALI MBAYA YA AFYA

KAHATA AWEKA MATUMAINI KWA KCB

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *