#Local News

INGONGA AILAUMU DCI, IPOA KWA UCHUNGUZI

Huku waathiriwa wa ukatili wa polisi wakisubiri haki, imebainika kwamba idara ya upelelezi wa jinai, DCI, na mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi, IPOA, zimekosa kuwasilisha faili za uchunguzi kwa afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma ili kuwafungulia mashtaka polisi wanaodaiwa kukiuka sheria.

Akizungumza jijini Nairobi alipokuwa akizindua mtaala kuhusu mashtaka ya ugaidi, mkurugenzi wa mashtaka ya umma Renson Ingonga, amesema nyingi ya kesi ambazo hazijawasilishwa kwake na taasisi hizo zinawahusu maafisa wa usalama.

Ameonya kuwa hatua hiyo itawaacha waathiriwa bila haki na washukiwa bila kesi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

INGONGA AILAUMU DCI, IPOA KWA UCHUNGUZI

KMPDU YATOA MAKATAA COAST GENERAL

INGONGA AILAUMU DCI, IPOA KWA UCHUNGUZI

VURUGU ZAWAACHA MAKUMI NA MAJERAHA KISII

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *