ATI ATI ZA KUAHIRISHA CAF 2027
Huenda dimba la mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao AFCON 2027 lililoratibiwa kuandaliwa na Kenya, Tanzania na Uganda likaahirshwa kutokana na ripoti kwamba mataifa hayo hayajajiandaa ipasavyo kuandaa dimba hilo.
Iwapo kipute cha mwaka ujao kitaahirishwa, shirikisho la soka barani Afrika CAF litalazimika kufutilia mbali Makala moja ya kipute hicho, linapojiandaa kuanzisha awamu mpya ambako AFCON itakuwa ikiandaliwa kila baada ya miaka 4 na wala si 2 ilivyo kwa sasa.
Kulingana na shirika la habari la kimataifa la The Guardian, uwezekano wa kuahirishwa kwa AFCON 2027 utajadiliwa hapo kesho katika kikao cha kamati kuu ya CAF jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.
Aidha, uwezekano wa kuhamisha maandilizi ya dimba la mataifa bingwa barani Afrika mwaka huu ya wanawake WAFCON 2026 kutoka Morocco hadi Afrika Kusini pia utajadiliwa na kuamuliwa.
Nchini Kenya, serikali imeimarisha maandalizi ya AFCON yam waka ujao, viwanja vya Nyayo na Kasarani vikiratibiwa kufungwa baada ya wikendi hii ili kufanikisha ukarabati.
Maafisa wa CAF wamewasili nchini ambako wanafanya ukaguzi wa viwanja na miundombinu nyingine kabla ya kuzuru Tanzania na Uganda kwa ukaguzi sawa.
Kenya imekariri kuwa iko tayari kuandaa dimba hilo, ingawa hofu za kiusalama viwanjani na ununuzi wa tiketi zimeibuliwa hasa kwa jinsi ilivyoshuhudiwa wakati wa kipute cha CHAN mwaka jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































