VIKOSI VYA SHUJAA, LIONESSES VYATAJWA
Wachezaji wapya ni sehemu ya kikosi cha wachezaji 12 wa timu ya taifa ya raga kwa wanaume Shujaa kilichotajwa, kujiandaa kwa mashindano ya HSBC SVNS Series wikendi hii katika uwanja wa Nyayo.
Miongoni mwa sura mpya kikosini ni David Nyangige, huku George Nyaoro akiwa nahodha akisaidiwa na Samuel Asati.
Wachezaji wengine ni John Okoth, Dennis Abukuse, Vincent Onyala, Kevin Wekesa, Patrick Odongo, Festus Shiasi, Nygel Amaitsa, Floyd Wabwire, na Christant Ojwang.
Kocha mkuu wa kikosi hicho Kelvin Wambua, ameelezea matumaini yake kwenye kikosi hicho, akisema kucheza mbele ya mashabiki nyumbani kutawapa msukumo mkubwa.
Huku hayo yakijiri, mwenzake wa timu ya wanawake Simon Odongo, amewajumuisha kikosini Marvel Oswago na Charity Nilah, wanaojiunga na Naomi Amumgumi, Maureen Muritu, nahodha Sheila Chajira, nahodha msaidizi Freshia Oduor, Sinaida Nyacho, Edith Nariaka, Grace Okulu, Stella Wafula na Phoebe Akinyi.
Katika mechi za ufunguzi, Shujaa watakabiliana na Canada, Uruguay, Belgium, Amerika na Ujerumani, huku Lionesses wakichuana na Brazil, Uchina, Argentina, Uhispania na Afrika Kusini.
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































